INSIDE INAPATIKANA MADUKANI

FILAMU YA JADA ITAKUWA SOKONI 19.02.2015

JADA IPO SOKONI

JADA IPO SOKONI

Thursday, August 16, 2012

WASANII WA BONGO MOVIE JB NA DOKII KUFANYA MAOMBI KATIKA KANISA LA MLIMA WA MOTO MIKOCHENI B ASSMBLES OF GOD

Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni B Assemblies of God hufanya mkesha kila Ijumaa, ambapo watu kutoka makanisa mbalimbali hujumuika kwa pamoja kwa umoja katika kumuomba Mungu. Mkesha hukusanya watu wengi sana na kama ni mara yako ya kwanza unaweza ukafikiri ni ibada ya Jumapili.

Katika mkesha huo kulikuwa na watu wengi sana na watu maaarufu katika nchi ya Tanzania walikusanyika pamoja kwa umoja kumuomba Mungu. Kulikuwa na wasanii wa Bongo Movie kama JB, Dokii na wengine wengi. Pia kulikuwa na waimbaji kama mlemavu wa miguu, Dayana Mwakatundu amabaye alitumbuiza wimbo wake ambao ulikonga mioyo ya watu.

Mchungaji Kingozi Dk. Getrude Rwakatare na Mchungaji wa Mkesha Prisca walitoa Neno la Mungu ili kuwaweka watu wa Mungu sawa wakati maombi yatakapoaanza.

Kwa wale waliohudhuria, mkono wa Mungu ulikuwa kwako, na walibarikiwa sana. Pia waliweza kuwaombea na wale ambao hawakuweza kufika katika mkesha huo na kuliombea Taifa la Tanzania.

Uongozi mzima wa kanisa la Mlima wa Moto unakukaribisha sana katika mkesha utakaofanyika Jumapili hii hapo kanisani kuanzia saa nne usiku na kuendelaea

Naomba sasa utazame yaliyoajili katika mkesha huo


Kanisa la Mlima wa Moto Mikocheni B Assemblies of God.

Mchungaji Getrude Rwakatare akitoa Neno wakati wa mkesha wa Ijumaa.Mchungaji wa mkesha Prisca akimsikiliza Mchungaji Kiongozi wakati wa Neno la Mungu.

Mwinjilisti Deo Taitas akiwa katika maombi.

Muumini wa kanisa la Mlima wa Moto akimuomba Mungu wake kwa yale anayopitia.

Kila mtu na shida yake, Mungu huwasikiliza wote.

Mwimbaji wa nyimbo za injilisti Dayana Mwakatundu akimwimbia Mungu wake wakati wa mkesha

Mwinjilisti Stanley Anko

Msanii wa Bongo Movie na Mwanamitindo Dokii akiwa katika ibada ya mkesha.

Msanii wa Bongo Movie, JB na mke wake wakijiandaa kuombewa.

Msanii wa Bongo Movie, JB akiombewa

Msanii wa Bongo Movie JB akiwa na mke wake

Maombi ya mkesha wa Ijumaa yakiendelea kanisani

Watu wakitembeatembea huku wakikemea kazi za shetani

Magoti yakipigwa na kila mtu akiwakilisha maombi yake kwa Mungu.

Baadhi ya waumini wakiwa katika eneo la madhabahu wakilia machozi.

Mchungaji kiongozi wa Mlima wa Moto, Dk. Getrude Rwakatare, naye akimlilia Mungu wake madhabahuni.

Mikono ikinyoshwa juu ili mradi Mungu asikie kilio chao.

Mzee wa kanisa Malya akiwa amelala katika eneo la mdhabahu akipeleka maombi yake kwa Mungu.I

No comments:

Post a Comment

There was an error in this gadget